London,England.
MWINGEREZA Anthony Joshua ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni mwamba wa miamba kwenye mchezo wa masumbwi ya uzito wa juu duniani baada ya usiku wa kuamkia leo Jumapili kufanikiwa kuutetea mkanda wake wa IBF na kujinyakulia mikanda ya IBO na WBA kwa kumchapa bondia mkongwe Wladimir Klitschko kwa TKO katika raundi ya 11 katika mpambano mkali uliofanyika kwenye Uwanja wa Wembley, London na kuhudhuriwa na watazamaji 90,000.Idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 80 iliyopita.
Katika mpambano huo ilishuhudiwa mabondia wote wawili wakiangushana chini kwa makonde mazito.Joshua alianza kumwangusha Klitschko katika raundi ya tano kabla ya yeye kuangushwa katika raundi ya sita na kuweka rekodi ya kuangushwa kwa mara ya kwanza katika mapambano yake 19 ya ndondi za kulipwa.
Joshua,27, ametangazwa mshindi baada ya majaji wawili Don Trella na Nelson Vazquez kumpa ushindi wa alama 96-93 na 95-93 huku Steve Weisfeld akimpa Klitschko,41,ushindi wa alama 95-93.
Ushindi huo umemfanya Joshua kuweka rekodi ya kucheza mapambano 19 na kushinda yote bila kupigwa ama kutoa sare pambano hata moja.
0 comments:
Post a Comment