Port Harcourt,Nigeria.
ZAMALEK ikiwa ugenini nchini Nigeria imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Enyimba katika mchezo mkali wa Kundi A wa kombe la klabu bingwa Afrika uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Adokiye Amiesimaka Stadium ulioko Port Harcourt,Nigeria.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa kwa kichwa dakika ya 8 na mshambuliaji hatari Bassem Morsy.
Katika mchezo mwingine wa Kundi A uliochezwa jana Jumamosi Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ikiwa ugenini Algeria iliichapa ES Setif kwa mabao 2-0 ya Tiyiani Mabunda na Khama Billiat.
0 comments:
Post a Comment