Lille,Ufaransa.
TIMU za taifa za Ufaransa na Uswisi zimeshindwa kutambiana baada ya usiku wa leo kutoka sare tasa ya bila kufungana katika mchezo mkali wa Kundi A wa michuano ya Ulaya/Euro uliochezwa katika uwanja wa Stade Pierre Mauroy huko mjini Lille.
Mpaka dakika tisini za mwamuzi Damir Skomina zinakwisha hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kuugusa wavu wa mwenzie.Ufaransa iliwapumzisha nyota wake Olivier Giroud na NG'olo Kante na kuwaanzisha Paul Pogba na Andre Pierre Gignac.
Kwa matokeo hayo Ufaransa na Uswisi kwa pamoja zimefanikiwa kutinga hatu ya 16 bora baada ya kumaliza nafasi ya kwanza na ya pili kutoka katika Kundi A.Ufaransa iko kileleni baada ya kujikusanyia alama saba,Uswisi iko nafasi ya pili ikiwa na alama tano.Timu zote zimecheza michezo mitatu kila moja.
Switzerland (4-2-3-1) Sommer;Lichtsteiner, Schar, Djourou, Rodriguez;Behrami, Xhaka; Shaqiri, Dzemalli,Mehmedi; Embolo.
France (4-3-3) Lloris; Sagna, Rami,Koscielny, Evra; Sissoko, Cabaye, Pogba;Coman, Gignac, Griezmann.
Katika mchezo mwingine wa kundi A uliochezwa huko Stade de Lyon Albania imeifunga Romania kwa bao 1-0 lililofungwa kwa kichwa dakika ya 43 na Armando Sadiku.Albania na Romania zimeaga michuano baada ya kumaliza zikiwa na pointi chache.
0 comments:
Post a Comment