728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 19, 2016

    CAF YATOA UFAFANUZI SUALA LA KESSY,HUENDA AKAIVAA MO BEJAIA LEO

    Cairo,Misri.

    Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika (CAF) limetoa ufafanuzi kuhusu uhalali wa klabu zinazoshiriki kombe la shirikisho kutumia wachezaji wake wapya waliosajiliwa.

    “Suala la kama hakuna malalamiko katika klabu anayotokea ni muhimu sana, baada ya hapo ni kuangalia kama usajili wa michuano hiyo umefuatwa.Kuna aina mbili, kwenye
    mtandao na kawaida.

    “Kama Caf imetoa leseni, kunakuwa hakuna shida. Lakini kunaweza kuwa na angalizo la kuangalia kama mchezaji hana mkataba tena na klabu aliyotokea au walimalizana kwa kufuata taratibu zote.

    “Kama atakuwa amemaliza mkataba na klabu aliyotokea, hakika hakuna tatizo hata kidogo na linaloangaliwa hapo ni hivi; usajili wa Caf umekamilika? Leseni imetoka? Kama hayo yametekelezwa hakuna tatizo,”

    SUALA LA HASSAN KESSY RAMADHANI NA WENGINE WAPYA

    Msemaji wa CAF Junior Binyam amefafanua:

    “Nimeambiwa Yanga wamezungumza na wenzetu wakati wa pre-match meeting kule Algeria, wameuliza maswali yote na kujibiwa vizuri na wameelewa.

    “Ninaamini wachezaji wao watakuwa hawana tatizo kwa maana ya usajili wa CAF. Kwenye suala la usajili katika klabu walizotoka, hili tunaweza kusubiri chama cha nchi yenu (TFF) ndiyo waseme. Lakini hadi sasa, inaonekana wachezaji hao wanaweza kutumika, hilo
    tuwaachie wao (Yanga).”

    Kwa kauli hiyo inaonekana Yanga, wana kila sababu ya kuwatumia Kessy, Juma Mahadhi,Andrew Vicent ‘Dante’ na Beno Kakolanya ambao wamesajiliwa.

    Sio mpaka Simba SC ama vilabu vingine wathibitishe hata TFF wanaweza fanya hivyo,hata bila ya uthibitisho kutoka upande wowote Yanga wanaweza kuwatumia ila kinachoonekana ni CAF walitoa tu angalizo kuwa Yanga wahakikishe wanawatumia wachezaji ambao wamekamilisha sajili pia wachezaji hao wawe hawana pingamizi zozote kutoka vilabu vyao walivyotoka.

    Lakini Obrey Chirwa raia wa Zambia atalazimika kusubiri wakati Yanga ikipambana kumtafutia usajili wake wa leseni kutoka Caf.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CAF YATOA UFAFANUZI SUALA LA KESSY,HUENDA AKAIVAA MO BEJAIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top