Waregem,Ubelgiji.
Mbwana Samatta ameendelea kupalilia kibarua chake katika klabu ya KRC Genk baada ya jana kuifungia bao moja katika ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya SV Zulte Waregem huko Regenboogstadion katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Ubelgiji Jupiler League.
Samatta ambaye katika mchezo wa jana alianza kikosi cha kwanza aliifungia KRC Genk bao la kuongoza dakika ya 8 tu ya mchezo kwa kichwa akiunganisha krosi ya nahodha Thomas Buffel toka wingi ya kulia.Hilo linakuwa ni bao la nne kwa Samatta kuifungia KRC Genk tangu alipojiunga nayo Januari mwaka huu.
Dakika ya 15 mlinzi wa SV Zulte Waregem,Marvin Baudry alijifunga katika harakati za kuokoa hatari langoni kwake na kuipatia KRC Genk bao la pili.
Zulte Waregem ilifanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 45 kupitia kwa M'Baye Leye.
Matokeo mengine ya Ligi hiyo:
SV Zulte Waregem 1-2 KRC Genk
Waasland Beveren 2-3 KV Kortrijk
KSC Lokeren 1-0 Sint Truidense VV
Mechelen 2-3 Sporting de Charleroi
Ligi kuu ya Ubelgiji itaendelea tena Jumanne Aprili 19 KRC Genk itakuwa nyumbani kuvaana na Club Brugge huku KV Oostende wao wakipimana ubavu na SV Zulte Waregem
0 comments:
Post a Comment