Manchester, England.
Manchester United wamepangwa kuwa wageni katika mchezo wao wa fainali wa kombe la FA dhidi ya Crystal Palace hapo Mei 21.
Katika mchezo huo utakaochezwa katika dimba la Wembley jijini London.Manchester United watavaa jezi nyeupe,bukta nyeusi na soksi nyeupe.Pia watatumia vyumba vya kubadilishia nguo ambavyo hutumiwa na timu ngeni.
Crystal Palace wao wamepewa heshima ya kuwa wenyeji katika mchezo huo hivyo watavaa jezi zao zilizozoeleka za rangi ya bluu na nyekundu.Pia watatumia vyumba vya kubadilishia nguo ambavyo hutumiwa na timu mwenyeji.
Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Manchester United kuvaa jezi nyeupe katika michuano ya mwaka huu ya kombe la FA.Mara ya kwanza ilikuwa ni katika mchezo wa raundi ya tano dhidi ya Shrewsbury Town kisha katika raundi ya sita katika mchezo dhidi ya West Ham United,
Manchester United na Crystal Palace zimetinga hatua ya fainali baada ya kupata ushindi katika michezo ya nusu fainali dhidi ya Everton na Watford.
0 comments:
Post a Comment