728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 19, 2016

    HIDDINK:WACHEZAJI CHELSEA WANAWAZA EURO TU

    London,England.

    Kocha wa muda wa klabu ya Chelsea Mdachi Guus Hiddink amesema kuvurunda kwa kikosi chake katika michezo ya hivi karibuni kumechangiwa na wachezaji wake kuwaza zaidi michuano ya Ulaya (Euro 2016) kuliko Ligi Kuu.

    Hiddink ametoa kauli hiyo zikiwa ni siku mbili tu tangu Chelsea ikubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa Manchester City katika mchezo wa ligi kuu England uliopigwa katika dimba la Stamford Blidge.

    Hiddink amesema "Siwezi kuwalaumu wachezaji kwa hiki kinachotokea sasa.Nadhani baadhi yao watakuwa wanahifadhi nguvu kwa ajili ya michuano ya Euro".

    Chelsea imepata ushindi mmoja tu katika michezo saba iliyopita na Hiddink anadhani michuano ya Euro itakayoanza mwezi Juni huko Ufaransa ndiyo inafanya wachezaji wake washindwe kuipigania timu kwa kuhofia kuumia ama kuchoka.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIDDINK:WACHEZAJI CHELSEA WANAWAZA EURO TU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top