Dar es salaam,Tanzania.
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm,amesema mshambuliaji wake Paul Nonga anakosa kujiamini na kucheza kutokana na presha ya mashabiki wa timu hiyo.
Akizungumza juzi, Pluijm alisema sababu hiyo inamweka katika wakati mgumu wa kuonyesha kiwango chake.
Pluijm alisema Nonga ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa uwanjani lakini ameshindwa kuonyesha kiwango chake
kutokana na presha za mashabiki naukubwa wa jina la klabu hiyo.
“Ni mchezaji mzuri anayejitambua, ana
nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja amekuwa mfano kwa wenzake kinachomkwamisha kukosa kujiamini,”alisema Pluijm.
Kocha huyo alisema anapenda kufanya kazi na mshambuliaji huyo lakini akiamini anaweza kubadilika.
“Wote tunakumbuka kuwa Nonga ni mshambuliaji mzuri mwenye uwezo mkubwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kucheza akiwa katika presha kubwa, lakini tuna imani atafanya vizuri,” alisema Pluijm.
Alisema pamoja na Nonga kushindwa kufanya kile anachomtuma uwanjani bado ataendelea kumtumia kwa kumpa nafasi ya kucheza katika kikosi chake.
“Yanga ni timu kubwa Afrika nani asiyejua kuichezea timu kama hii ni bahati, ina mamilioni ya mashabiki hilo lazima utambue ndio maana Nonga amekuwa katika wakati mgumu.”
CHANZO:BINGWA
0 comments:
Post a Comment