Milan,Italia.
Mario Balotelli amesema hataki tena kurudi kuichezea Liverpool pindi mkataba wake wa mkopo AC Milan utakapokuwa umekwisha mwishoni mwa msimu huu.
Balotelli, 25, ambaye ameifungia AC Milan mabao matatu katika michezo 19 ya Ligi ya Seria A amesema anataka kuitumia michezo michache iliyobaki ili kujihakikishia nafasi ya kubaki San Siro.
"Ninachokitaka kwa sasa ni kubaki AC Milan.Akili yangu imetulia hapa.Alisema Balotelli muda mfupi baada ya kuongoza AC Milan kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Sampdoria juzi Jumapili.
"Sikuwa na furaha Liverpool hivyo sitaki kurudi tena hapo.Nimefanya vizuri katika michezo miwili iliyopita bado kuna michezo mingine sita ya kuonyesha uwezo wangu.
Balotelli alijiunga na Liverpool mwaka 2014 kwa ada ya 16m akitokea AC Milan lakini baada ya mambo kumuendea vibaya Anfield,Agosti 2015 alirejea AC Milan kwa mkopo wa msimu mmoja huku kukiwa na kipengele cha kununuliwa moja kwa moja kwa £7m.
Wakati huohuo taarifa kutoka Italia zinasema mmiliki wa klabu ya Monaco Dmitry
Rybolovle amekutana na Balotelli kujaribu kumshawishi nyota huyo ajiunge na klabu yake msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment