London,England.
BADO KIDOGO TU!!Leceister City inahitaji kushinda mchezo mmoja kati ya mitatu iliyobakia ili iweze kutwaa ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu England hii ni baada ya Jumatatu usiku washindani wao wa karibu Tottenham Hotspur kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1West Bromwich Albion nyumbani White Hart Lane,London na kufanya tofauti ya pointi kati yao ziwe saba.
Tottenham Hotspur iliyoonekana kuwa mpinzani wa kweli wa Leceister City ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 32 kipindi cha kwanza baada ya mlinzi wa West Bromwich Albion Craig Dawson kujifunga wakati akijaribu kuokoa mpira wa faulo uliopigwa na Christian Ericksen.
Dakika ya 73 Craig Dawson aliisawazishia bao West Bromwich Albion baada ya kuunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Craig Gardner na kufanya mchezo uishe kwa sare ya bao 1-1.
Kutokana na matokeo hayo Leceister City inahitaji kupata pointi tatu tu katika michezo mitatu iliyobaki ili iweze kutwaa ubingwa wa kwanza wa ligi kuu baada ya kuusubiri kwa kipindi cha miaka 132.
Jumapili Leceister City itakuwa mgeni wa Manchester United huku Jumatatu Tottenham Hotspur wao watasafiri kwenda kuvaana na Chelsea huko Stamford Blidge na ikiwa watapoteza mchezo huo basi sare yoyote dhidi ya Manchester City itaiwezesha Leceister City kuwa mabingwa.
0 comments:
Post a Comment