Manchester,England.
Mabao mawili ya kinda Mnigeria
Kelechi Ihenaicho na mengine ya Fernando Reges na Sergio Aguero yameiwezesha
Manchester City kutoka kifua mbele nyumbani Etihad baada ya kuichapa Stoke City
kwa mabao 4-0 katika mchezo mkali wa Ligi kuu England uliopigwa mchana wa leo.
Manchester City ilianza kuandika
bao la kuongoza dakika ya 35 tu ya mchezo kupitia kwa kiungo wake Fernando
Reges.Fernando alifunga bao hilo kwa kichwa akimalizia krosi safi ya winga
Jesus Navas.Dakika ya 43 Sergio Aguero aliifungia Manchester City bao la pili
kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya Kelechi Iheanacho kuangushwa kwenye
eneo la hatari.
Dakika ya 64 Kelechi Iheanacho
aliifungia Manchester City bao la tatu kabla ya kuongeza la nne dakika ya
74.Kufuatia ushindi huo Manchester City imefanikiwa kurejea nafasi ya tatu
baada ya kufikisha pointi 64 na kuishusha Arsenal mpaka nafasi ya nne ikiwa na
pointi zake 63.
0 comments:
Post a Comment