Yanga imetoka nyuma na kuichapa Mgambo JKT mabao 2-1 katika mchezo mkali wa kiporo wa ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Mgambo JKT ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Bolly Shaibu kufunga dakika ya 4 baada ya kuuwahi mpira uliomshinda Salum Telela.
Dakika ya 43 Deus Kaseke aliifungia Yanga bao la kusawazisha baada ya kupokea pasi ya kichwa toka kwa Hamis Tambwe.
Kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Paul Nonga na kumuingiza Donald Ngoma aliyeongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa Mgambo JKT.
Dakika ya 72 mpira wa kichwa wa Hamis Tambwe uliotemwa na kipa wa Mgambo ulimkuta Deus Kaseke katika nafasi nzuri na kuiandikia Yanga bao la pili.
Kufuatia ushindi huo Yanga imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu bars baada ya kufikisha pointi 62 kufuatia kushuka dimbani Mara 24.
0 comments:
Post a Comment