728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 27, 2016

    DAKIKA 45 ZA FARID MUSSA ZAIPAGAWISHA WAHISPANIA,WAMUULIZA SWALI LA KIZUSHI

    Tenerife,Hispania.

    WINGA chipukizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC,Farid Mussa, aliyeko majaribioni
    nchini Hispania, jana aliiongoza CD Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza
    nchini humo ‘Segunda Division’ kuichapa UD Diabora bao 1-0.

    Habari njema zaidi kuhusu Farid ni winga huyo kufanya vizuri katika
    mtihani wake huo wa kwanza baada ya kuwapagawisha viongozi na benchi la ufundi la Tenerife.

    “Naendelea vizuri sana na jana usiku nilicheza dakika 45 katika mchezo wa
    kirafiki na nimeiongoza timu hiyo kupata ushindi, nimefanikiwa kuivutia
    hii timu kwani walishangazwa na
    kiwango changu kizuri hadi kudiriki kuniuliza kama kweli mimi ni Mtanzania baada ya mechi hiyo,”
    alisema Farid wakati akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz.

    Kwa mujibu wa wakala wa Farid, John Sorzano raia wa Venezuela aliyeishi sana nchini England, amedai kuwa wiki ijayo nyota huyo anatarajia kuanza rasmi majaribio katika timu
    mbili za Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’akianzia Las Palmas na kumalizia
    Malaga.

    Farid atafanya majaribio hayo na kukaa huko kwa wiki mbili zijazo akitarajiwa kurejea nchini Mei 19
    mwaka huu wakati msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakapokuwa umemalizika.

    Lakini mechi pekee ambayo anaweza kuiwahi ni ile ya fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) itakayofanyika Mei 25 mwaka huu, ambayo Azam FC ilitinga juzi kwa kuichapa Mwadui ya Shinyanga na itacheza na mshindi wa nusu fainali
    nyingine kati ya Yanga na Coastal Union..


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DAKIKA 45 ZA FARID MUSSA ZAIPAGAWISHA WAHISPANIA,WAMUULIZA SWALI LA KIZUSHI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top