London,England.
Bao la dakika ya 93 la mshambuliaji Mfaransa Antony Martial limetosha kuipeleka Manchester United katika fainali ya kombe la kombe la FA Cup baada ya usiku wa leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Everton katika mchezo mkali wa nusu fainali uliochezwa katika dimba la Wembley jijini London.
Manchester United ilianza kupata bao la kuongoza dakika ya 34 kupitia kwa Marouane Fellaini kabla ya Everton kusawazisha dakika ya 75 baada ya Chris Smaillng kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Louis Van Gaal ya kumtoa Marouane Fellaini na kumuingia Ander Herrara yaliifaidisha Manchester United baada ya kiungo huyo Mhispania kuwazidi ujanja walinzi wa Everton na kutoa pasi nzuri kwa Antony Martial aliyeifungia Manchester United bao la ushindi dakika ya 93.
Kesho Jumapili nusu fainali ya pili ya FA Cup itachezwa ambapo Crystal Palace itavaana na Watford na mshindi atacheza na Manchester United katika mchezo wa fainali hapo mwezi Mei.
0 comments:
Post a Comment