Liverpool,England.
Liverpool imemfungia kwa muda usiojulikana beki wake Mfaransa Mamadou Sakho baada ya kumkuta na hatia ya kutumia madawa yanayodhaniwa kuwa ni ya kuongeza nguvu.
Sakho,26 amekutwa na hatia hiyo leo mchana baada ya vipimo vya afya kuonyesha kuwa beki huyo wa zamani Paris Saint Germain ametumia dawa iitwayo ‘fat burner’ pasipo kushauriana na jopo la madaktari wa klabu hiyo.
Fat burner ni dawa maalumu kwa kupunguza uzito.Sakho amepewa mpaka jumanne kukubali kosa au kuomba kufanyiwa vipimo kwa mara nyingine.
Kwa kuanzia Liverpool imemuondoa Sakho katika kikosi chake kitakachovaana na Newcastle United jioni ya leo huku pia ikianza uchunguzi wa kina kujua kiini cha kadhia hiyo.
0 comments:
Post a Comment