728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 29, 2016

    GEORGE WEAH AUTAKA TENA URAIS WA LIBERIA

    Monrovia,Liberia.

    Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Chelsea, AC Milan na Paris Saint-Germain George Opong Weah ametangaza kuwa atagombea kwa mara ya pili Urais wa nchi yake ya Liberia katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2017.

    Akitangaza azma hiyo Weah,49 aliyewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka 1995 amesema anataka kuibadili na kuipa maisha bora nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

    Weah ameongeza kuwa akipata ridhaa ya kuiongoza Liberia atatilia mkazo masuala ya Elimu,Afya,Maji,Umeme,Ajira na kuondoa Umasikini.

    Mara ya kwanza Weah kugombea Urais wa Liberia ilikuwa ni mwaka 2005 alipobwagwa na Mwanamama Ellen Johnson Sirleaf ambaye ukomo wake wa uongozi unaishia mwaka 2017.

    Kwa mujibu wa sheria za Liberia Ellen Johnson Sirleaf hataruhusiwa tena Urais kwani tayari ameshaongoza kwa vipindi viwili.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: GEORGE WEAH AUTAKA TENA URAIS WA LIBERIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top