Villarreal,Hispania.
Bao la dakika ya 90 la Adrian Lopez limeipa Villarreal ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Liverpool katika mchezo mkali wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Europa Ligi uliopigwa katika dimba la El Madriga,Hispania.
Lopez alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Denis Suarez aliyeingia ndani katika eneo la hatari la Liverpool.
Ushindi huo ni wa saba kwa Villarreal kuupata nyumbani katika michuano hiyo msimu huu.Katika mchezo huo Liverpool ilimiliki mpira kwa asilimia 52 na kufanikiwa kupata kona 3,Villarreal wao walimiliki mpira kwa asilimia 48 na kufanikiwa kupata kona 7.
Katika mchezo mwingine wa Europa Ligi mabingwa watetezi Sevilla wamejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga fainali ya tatu mfululizo baada ya kulazimisha sare ya 2-2 ugenini dhidi ya Shakhtar Donetsk huko Arena Lviv,Ukraine.
Mabao ya wageni Sevilla yamefungwa na Vitolo pamoja na Kevin Gameiro kwa mkwaju wa penati huku wenyeji Shakhtar Donetsk wakipata mabao yao kupitia kwa Marlos na Taras Stepanenko.
0 comments:
Post a Comment