Dar es salaam,Tanzania.
Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA), kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa MZFA na makamu mwenyekiti wa FAT Silvanus Makalu Ngofilo aliyefariki dunia juzi jijini Mwanza.
Katika salamu zake, TFF imewapa pole familia ya marehemu Ngofilo ndugu, jamaa,marafiki, wadau wa mpira wa miguu kanda ya Ziwa na kusema Shirikisho liko pamoja nao katika kipindi hiki cha maomblezo.
Mazishi ya Silvanus Makalu Ngofilo yatafanyika kesho Jumapili kijijini kwao Mwamanyili, Wilayani ya Busega mkoa wa Shinyanga ambapo TFF itawakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Vedasto Lufano.
Marehemu Ngofilo wakati wa uhai wake aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa FAT wakati wa Muhidin Ndolanga na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya FAT, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA) 1984-1994, ambapo baada ya kustaafu alipewa wenyekiti wa heshima na MZFA.
0 comments:
Post a Comment