728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 28, 2016

    ATLETICO MADRID YAICHAPA BAYERN MUNICH LIGI YA MABINGWA ULAYA

    Madrid,Hispania.

    Bao la dakika ya 11 la kipindi cha kwanza la kiungo Saul Niguez,21 limeiwezesha Atletico Madrid kuichapa Bayern Munich bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

    Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Vicente Calderon jijini Madrid pasi safi ya Augusto Fernandez ilimkuta Saul Niguez katika nafasi nzuri na kufanikiwa kuihadaa ngome ya ulinzi ya Bayern Munich kabla ya kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango Manuel Neuer na kuipatia Atletico Madrid bao hilo pekee.

    Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo huko Allianz Arena,Ujerumani na mshindi atakata tiketi ya kucheza fainali dhidi ya mshindi kati ya Real Madrid ama Manchester City.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ATLETICO MADRID YAICHAPA BAYERN MUNICH LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top