Napoli,Italia.
Staa wa zamani wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Argentina Diego Armando Maradona amemwagia sifa kemkem mlinzi mahiri wa Napoli Kalidou Koulibaly na kufichua ni kwanini mlinzi huyo toka Senegal hatupiwi macho na vilabu vikubwa.
Koulibaly ambaye ni raia wa Senegal amekuwa nguzo ya safu ya ulinzi ya Napoli kiasi cha kutajwa kuwa mmoja kati ya walinzi bora zaidi wa Seria A kwa msimu huu.
Maradona akiongea na kituo cha habari cha Piuenne cha nyumani kwao Argentina amesema " Koulibaly amekuwa katika kiwango bora sana msimu huu bila shaka yeye ndiye mlinzi bora zaidi kwa sasa Seria A.Hazungumzwi sana Italia kwa sababu amezungukwa na ubaguzi mkubwa wa rangi.
Maradona ameongeza "Kwa kiwango alichokionyesha Koulibaly msimu huu basi kama angekuwa Mzungu leo hii angekuwa anachezea Real Madrid au Barcelona lakini kwa sababu ni Mwafrika hakuna klabu yoyote kubwa inayomuongelea.
Wakati huohuo Maradona ameipongeza Juventus kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wake wa tano mfululizo wa Seria A baada ya Napoli kuchapwa na AS Roma kwa bao 1-0 jana jumatatu.Lakini ameonya kuwa licha ya Juventus kuwa na kikosi bora,waamuzi wameisaidia sana kuirahisishia kazi,imebebwa.
0 comments:
Post a Comment