Manchester, England.
Manchester United imetajwa kuwa ni klabu iliyotumia pesa nyingi zaidi kuwalipa mawakala wa wachezaji kuliko vilabu vingine vyote vya ligi kuu nchini England katika kipindi cha kati ya Octoba 1 2015 na Februari 1,2016.
Katika ripoti hiyo iliyotolewa siku ya Ijumaa Manchester United imeripotiwa kutumia zaidi ya £10m licha ya kushindwa kufanya usajili wowote katika kipindi hicho huku pia ikishindwa kuwapa mikataba mipya nyota wake mbalimbali.
Katika kipindi cha Octoba mpaka Februari Manchestet United imefanikiwa kuwauza Ben Pearson na Liam Grimshaw kwenda Preston huku ikitoa kwa mkopo jumla ya nyota wake sita wakiwemo mshambuliaji James Wilson na mlinda mlango Victor Valdes.
Vilabu vingine vilivyotajwa kumwaga pesa kwa ajili ya kulipa ada za mawakala ni Liverpool, Manchester City na Arsenal.
Orodha kamili iko kama ifuatavyo:
1. Manchester United £10,023,318
2. Liverpool £6,672,713
3. Manchester City £5,880,098
4. Arsenal £3,135,483
5. West Ham United £2,691,331
6. Tottenham £2,562,853
7. Chelsea £2,214,227
8. Stoke City £1,748,093
9. West Bromwich Albion £1,700,127
10. Aston Villa £1,638,571
11. Bournemouth £1,451,647
12. Crystal Palace £1,197,845
13. Norwich £1,183,890
14. Leicester £936,004
15. Southampton £799,750
16. Watford £782,494
17. Sunderland £733,894
18. Newcastle £538,107
19. Swansea £491,000
20. Everton £471,400
0 comments:
Post a Comment