Drogba akishangilia bao lake.
Chicago,Marekani.
Didier Drogba ameendelea kuonyesha kuwa ujuzi hauzeeki baada ya kutokea benchi na kuifungia Montreal Impact bao la kusawazisha kwa kisigino katika ushindi wa mabao 2-1ugenini dhidi ya Chicago Fire katika mchezo mkali wa Ligi ya MSL uliopigwa katika dimba la Toyota Park,Chicago alfajiri ya leo.
Drogba,38 akicheza mchezo wake wa kwanza wa msimu baada ya kukosa michezo minne ya awali kutokana na kuchezwa katika viwanja vyenye nyasi bandia [artificial turf] aliifungia Montreal
Impact bao hilo dakika ya 56 zikiwa ni dakika sita tangu aingie uwanjani akitokea benchi.
Drogba aliifunga bao hilo akiunganisha pasi ya Dominic Oduro na kufanya matokeo yawe 1-1 baada ya wenyeji Chicago Fire kutangulia kupata bao la kuongoza dakika ya 29 kupitia kwa Kennedy Igboananike.
Mchezo ukiwa unaelekea ukingoni Muargentina Ignacio Piatti aliifuingia Montreal Impact bao la ushindi dakika ya 91 kwa mkwaju mkali wa mbali baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Dominic Oduro.
Kufuatia ushindi huo Montreal Impact imeendelea kukaa kileleni katika msimamo wa ukanda wa Eastern Conference ikiwa imejikusanyia pointi 12.
0 comments:
Post a Comment