Madrid,Hispania.
Ndoto za winga Cristiano Ronaldo kuichezea klabu yake ya Real Madrid katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City Jumatano ijayo huenda zikayeyuka baada ya vipimo vya MRI Scan kuonyesha kuwa Staa huyo wa Ureno amechanika msuli wa mguu.
Ronaldo,31 ambaye hakuwepo katika mchezo wa kwanza uliopigwa Etihad,Manchester siku ya Jumanne na kuisha kwa sare ya bila kufungana ameripotiwa kuwa mbali ya kukosa mchezo huo wa marudiano pia atakosa michezo kadhaa ya Ligi ya La Liga.
Kukosekana kwa Ronaldo itakuwa ni pigo kubwa sana kwa Real Madrid inayopambana kutwaa taji la kumi na moja la ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Wakati huohuo taarifa kutoka jijini Madrid zinasema Ronaldo atafanyiwa kitu kinachoitwa stem cell kwa ajili ya kumfanya apone haraka jeraha hilo na hatimaye aweze kuikabili Manchester City siku ya Jumatano.
0 comments:
Post a Comment