Roma,Italia.
JUVENTUS imefanikiwa kutwaa ubingwa wa tano mfululizo wa ligi ya Serie A baada ya leo jioni wapinzani wao wa karibu Napoli kuchapwa bao 1-0 na AS Roma katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Stadio Olimpico jijini Roma.
Bao la dakika ya 89 la kiungo wa AS Roma Radja Nainggolan limeifanya Juventus itangaze ubingwa kwa tofauti ya pointi 12 dhidi ya washindani wao wa karibu Napoli huku kila timu ikiwa na michezo mitatu mkononi.Juventus imefikisha pointi 85 huku Napoli ikibaki na pointi zake 73.
Ubingwa huo unakuwa wa 34 kutwaliwa na Juventus huku ukiwa ni ubingwa wake wa tano katika kipindi cha miaka mitano.
Mpaka inafanikiwa kutwaa ubingwa wa SeriA Juventus imepoteza mchezo mmoja peke yake hii ikiwa ni Octoba 28 mwaka jana ilipochapwa bao 1-0 na Sassuolo.
Radja Nainggolan akishangilia bao lake dhidi ya AS Roma jioni ya leo.
0 comments:
Post a Comment