Barcelona,Hispania.
UTOTO!!Hii ndiyo kauli pekee unayoweza kuitumia kuelezea tukio lisilo la kiungwana alilolifanya Neymar Jr jana jumapili dhidi ya mlinzi wa kulia wa Valencia Antonio Barragan.
Habari ni kwamba Staa wa FC Barcelona Neymar Jr huenda akakumbana na adhabu kali toka kwa chama cha soka cha Hispania baada ya picha za Televisheni kumuonyesha staa huyo wa Brazil akimchapa kofi usoni mlinzi wa kulia wa Valencia Antonio Barragan.
Neymar Jr alifanya tukio hilo baasa ya mchezo kuwa umemalizia na FC Barcelona kulala kwa mabao 2-1 toka kwa Valencia nyumbani Camp Nou.
Neymar alimvizia Barragan aliyekuwa akishangilia ushindi na wachezaji wenzake wa Valencia na kumchapa kofi hali iliyofanya Barragan aje juu kabla ya kuamuliwa na wachezaji waliokuwa karibu yake.
Hivyo kwa kuwa tukio hilo halikuweza kuonwa na mwamuzi wa mchezo huo David Fernandez Borbalan chama cha soka cha Hispania kitalazimika kutumia picha za Televisheni ili kumuadhibu Neymar Jr.
0 comments:
Post a Comment