728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 25, 2016

    MAHREZ ATWAA UCHEZAJI BORA LIGI KUU ENGLAND

    London,England.

    Winga wa Leicester City Mualgeria Riyad Mahrez ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu England maarufu kama PFA Player of the Year kwa msimu wa 2015-16 katika hafla maalumu iliyofanyika jumapili usiku huko Grosvenor House,jijini London.

    Mahrez,25 ametwaa tuzo hiyo baada ya kufanikiwa kuifungia Leceister City mabao17 huku akitengeneza mengine 11katika michezo 33 ya ligi kuu msimu huu.

    Nyota huyo wa zamani wa Le Havre ameibuka mshindi kwa kuwabwaga Jamie Vardy,N'Golo Kante,Harry Kane,Dimitri Payet na Mesut Ozil.

    Tuzo ya mchezaji bora kijana imeenda kwa kiungo wa Tottenham Dele Alli,20.Alli ametwaa tuzo hiyo hiyo akiwashinda Harry Kane,Phillipe Coutinho na Romelo Lukaku.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAHREZ ATWAA UCHEZAJI BORA LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top