728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 27, 2016

    DELE ALLI MATATANI ENGLAND,UBONDIA WAMPONZA

    London,England.

    Kiungo mahiri wa Tottenham na mshindi wa tuzo ya PFA Muingereza Dele Alli anakabiliwa na hatari ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi kuu England na chama cha soka nchini humo FA kwa kosa la kumpiga ngumi ya tumbo kiungo wa West Bromwich Albion Claudio Yacob.

    Alli alifanya tukio hilo lisilo la kiuwana michezo Jumatatu usiku,dakika ya 26 katika mchezo ambao klabu yake ya Tottenham ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na West Bromwich Albion nyumbani White Hart Lane.

    FA imemtia hatiani Alli kwa kutumia ushahidi wa picha za Televisheni kwa kuwa mwamuzi wa mchezo huo hakuweza kuliona tukio hilo ambalo adhabu yake ilikuwa na kadi nyekundu ya moja kwa moja.

    Ikiwa Alli atakumbwa na adhabu hiyo atakosa michezo yote iliyobaki ya ligi kuu England.Michezo hiyo ni dhidi ya Chelsea,Southampton na Newcastle United.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DELE ALLI MATATANI ENGLAND,UBONDIA WAMPONZA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top