Geneva,Uswisi.
SHIRIKISHO la soka ulimwenguni,FIFA,leo mchana limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka kwa mwezi Agosti.
Katika orodha hiyo Tanzania imeshuka kwa nafasi nane kutoka nafasi ya 124 mwezi Julai hadi nafasi ya 132.Hii inatokana na kufanya vibaya katika mchezo wake wa mwisho wa michuano ya kusaka tiketi ya kufuzu AFCON.
Wakati Tanzania ikishuka kwa nafasi hizo nane majirani zao,Uganda,ambao hivi karibuni wamefuzu michuano ya AFCON wao wamebaki katika nafasi yao ya 65 duniani na 15 barani Afrika.
Barani Afrika Ivory Coast imeendelea kubakia katika nafasi ya kwanza huku kidunia ikiwa nafasi ya 34.Nafasi ya pili imeshikwa na Algeria kidunia ni ya 35,Senegal ni ya tatu na Ghana ni ya nne.
Washindi wa tatu wa Olimpiki Nigeria wamepanda kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 67 mpaka nafasi ya 64 kidunia.Afrika iko nafasi ya 14.
Kidunia Argentina imeendelea kuongoza orodha hiyo ikifuatiwa kwa ukaribu na Ubelgiji iliyo katika nafasi ya pili,Ujerumani ni ya tatu,Colombia ni ya 4,Brazil ni ya 5 ikiwa imepanda kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 10.
Mabingwa wa Ulaya Ureno wameshika nafasi ya 7 kidunia.Ulaya wako nafasi ya 3.Ufaransa ni ya 4 Ulaya,Kidunia ni ya 8.Wales iko nafasi ya 10 kidunia,Ulaya ni ya 5.
0 comments:
Post a Comment