Abuja,Nigeria.
WANIGERI bado hawajakata tamaa ya kumshawishi winga wa zamani wa Liverpool,Jordan Ibe,akubali kuichezea timu yao ya taifa ya Super Eagles.
Ibe,20,ambaye kwasasa anaichezea FC Bournemouth ,mapema mwaka jana alikataa wito wa kuichezea Nigeria katika michezo ya kuwania tiketi ya AFCON pale alipoombwa kufanya hivyo na aliyekuwa kocha wa wakati huo,Sundey Oliseh.
Akiongea na Soka Extra mjumbe mmoja wa kamati ya ufundi ya chama cha soka cha Nigeria (NFF) ,ambaye hakutaka jina lake litajwe,amekiri kuwa NFF bado haijakata tamaa ya kumshawishi Ibe ili akubali kuichezea Nigeria ambayo ni nchi ya asili ya baba yake.
Mjumbe huyo amesema kuwa Ibe hakukataa moja kwa moja kuichezea Nigeria bali aliomba apewe muda zaidi wa kufikiria kabla ya kufikia uwamuzi.
Kwasasa Ibe anachezea timu ya taifa ya England ya vijana waliochini ya umri wa miaka 21na ameripotiwa kuwa alikataa wito wa kuichezea Nigeria kwa mategemeo ya siku moja kuja kuichezea timu ya taifa ya wakubwa ya England.
0 comments:
Post a Comment