728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 15, 2016

    ZANZIBAR YAPOTEZA TENA CECAFA SAFARI HII YAGONGWA 11 -0


    Jinja,Uganda.

    TIMU ya taifa ya wanawake ya Zanzibar,Zanzibar Queens,imeiaga kinyonge michuano ya CECAFA ya wanawake inayoendelea huko Jinja nchini Uganda,baada ya mchana huu kukubali kichapo cha mabao 11 toka kwa Kenya katika mchezo wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa FUFA Technical Center.

    Huu ni mchezo wa tatu kwa Zanzibar Queens kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao kwani katika mchezo wake wa kwanza ilifungwa mabao 10-1 na Burundi,ikachapwa mabao 9-0 na Uganda.Jumla imefungwa mabao 30 huku ikiambulia kufunga bao moja pekee.

    Kenya imejipatia mabao hayo kupitia kwa Christine Nafula,Jacky Nedy,Atieno,Ogol Mercy Achieng,Esse Akidi na Corazone Aquino. 

    Kwa matokeo hayo Kenya inaungana na Tanzania pamoja na Ethiopia kufuzu hatua ya nusu fainali huku zikisubiri mshindi kati ya Uganda na Burundi kukamilisha idadi ya timu nne za hatua hiyo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ZANZIBAR YAPOTEZA TENA CECAFA SAFARI HII YAGONGWA 11 -0 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top