Rotterdam,Uholanzi.
MENEJA wa Manchester United,Mreno Jose Mourinho,amefanya mabadiliko manane kutoka katika kikosi kilicholazwa mabao 2-1 na Manchester City Jumamosi iliyopita tayari kwa mchezo wa leo usiku wa michuano ya Europa Ligi dhidi ya Feyenoord.
Katika mabadiliko hayo Marcus Rashford ambaye katika mchezo dhidi ya Manchester City alianzia benchi kabla ya kuingia kipindi cha pili amepewa jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji akishirikiana na Antony Martial huku mkongwe Zlatan Ibrahimovic akiachwa benchi.
David De Gea,Eric Bailly na Paul Pogba ndiyo wachezaji pekee ambao hawakuguswa na mabadiliko hayo.Wayne Rooney na Luke Shaw wao hawatakuwepo kabisa kikosini kwani hawakusafiri na timu kwenda Uholanzi.
Kikosi kitakachoanza usiku huu kiko kama ifuatavyo:
XI:De Gea, Darmian, Bailly,Smalling, Rojo, Schneiderlin, Herrera, Mata,Pogba, Martial, Rashford.
Akiba:Romero, Fosu-Mensah, Carrick,Fellaini, Depay, Young, Ibrahimovic.
0 comments:
Post a Comment