Jinja,Uganda.
WENYEJI Uganda wamefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya CECAFA ya wanawake baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burundi katika mchezo wa mwisho wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa Njeru Technical Centre huko Jinja,Uganda.
Bao pekee la mchezo huo uliokuwa mgumu kutokana na timu zote kucheza kwa tahadhari ya kuogopa kupoteza mchezo limefungwa na Fazirah Ikwaput kwa kichwa dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.
Ikwaput alifunga bao hilo akimalizia krosi safi toka kwa Sseninde na kumfunga kipa wa Burundi,Belinda Ndoreraho.
Timu ambazo zimefanikiwa kutinga nusu fainali ni Tanzania,Uganda,Kenya na Ethiopia.
0 comments:
Post a Comment