728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 15, 2016

    AKINA SAMATTA WAANZA VIBAYA MAKUNDI EUROPA LIGI


    Vienna,Austria.

    KLABU ya KRC Genk inayochezewa na Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania,Mbwana Samatta,imeianza vibaya hatua ya makundi ya michuano ya Europa Ligi baada ya usiku huu kufungwa mabao 3-2 na Rapid Viena katika mchezo mkali wa kundi F uliochezwa katika uwanja wa Allianz Stadion huko Vienna,Austria.

    KRC Genk ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 29 kupitia kwa Leon Bailey.Bailey alifunga bao hilo baada ya kumegewa pasi safi na Mbwana Samatta.

    Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko KRC Genk ilikuwa inaongoza kwa bao hilo moja.Kipindi cha pili wenyeji Rapid Viena walikuja na nguvu mpya na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 51 kupitia kwa Stefan Schwab kisha la pili dakika ya 59 kupitia kwa Joelinton na la tatu dakika ya 60 kupitia kwa Omar Colley aliyejifunga.

    Mnamo dakika ya 90 ya mchezo Leon Bailey aliifungia KRC Genk bao la pili na kufanya mchezo uishe kwa sare ya mabao 3-2.

    Katika mchezo mwingine wa kundi hilo la A uliochezwa huko Stadio Citta del Italia,Sassuolo wameichapa Atletico Madrid kwa mabao 3-0.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AKINA SAMATTA WAANZA VIBAYA MAKUNDI EUROPA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top