Rotherdam, Uholanzi.
MANCHESTER United imepoteza mchezo wa pili ndani ya siku tano baada ya usiku huu kufungwa bao 1-0 na Feyenoord katika mchezo wa hatua ya makundi ya michuano ya Europa Ligi.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa De Kuip huko Rotherdam, Uholanzi,wenyeji Feyenoord,walipata bao lao kupitia kwa Tonny Vilhena katika dakika ya 76.
Vilhena alifunga bao hilo akiunganisha krosi ya Nicolai Jørgensen.
Hicho ni kichapo cha pili kwa Manchester United ndani ya siku tano baada ya Jumamosi iliyopita kuchapwa mabao 2-1 na mahasimu wao Manchester City huko Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment