Barcelona,Hispania.
BARCELONA imezianza vyema harakati zake za kuusaka ubingwa wa Ulaya iliyoupoteza msimu uliopita kwa mahasimu wao Real Madrid baada ya usiku huu kuifunga Celtic kwa mabao 7-0 katika mchezo wa kwanza wa kundi C wa hatua ya makundi uliochezwa katika uwanja wa Camp Nou.
Mabao ya Barcelona yamefungwa na Lionel Messi aliyefunga mabao matatu,Luis Suarez aliyefunga mabao mawili
Mabao mengine yamefungwa na Neymar pamoja na Andres Iniesta.
Katika mchezo mwingine uliochezwa huko Parc des Ufaransa Arsenal imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Paris Saint Germain.
Paris Saint Germain ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 1 ya mchezo kupitia kwa Edinson Cavani.Alexis Sanchez aliisawazishia Arsenal kwa mkwaju mkali dakika ya 78.
Wachezaji Olivier Giround wa Arsenal na Marco Verratti wa Paris Saint Germain walionyeshwa kadi nyekundu kwa kuleteana ubabe.
MATOKEO MENGINE
Basel 1-1 Ludogorets Razgrad
Dynamo Kyiv 1-2 Napoli
Bayern München 5-0 Rostov
PSV Eindhoven 0-1 Atlético Madrid
Benfica 1-1 BeÅŸiktaÅŸ
Manchester City P-P Borussia Mönchengladbach
0 comments:
Post a Comment