Barcelona, Hispania.
JANA Jumanne usiku Lionel Messi alifunga hat-trick yake ya sita katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga hat-trick nyingi zaidi katika historia ya michuano hiyo pale alipoiongoza Barcelona kuichapa Celtic kwa mabao 7-0 katika mchezo wa kundi C uliochezwa Camp Nou.
Hat-trick hiyo ya dakika za 3, 27, 60 imemfanya Messi,27,kuwa mbele ya mpinzani wake Cristiano Ronaldo,31,mwenye hat-trick tano mpaka sasa.
Pia hat-trick hiyo imemfanya Messi kufikisha mabao 50 katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa.Bao moja zaidi ya Cristiano Ronaldo na sawa na nyota wa zamani wa Manchester United,Ruud van Nistelrooy.
Sasa Messi anahitaji kufunga mabao matatu zaidi ili kuweza kuifikia rekodi ya nyota wa zamani wa Real Madrid,Raul Gonzalez,ya kufunga mabao 53 katika michezo ya hatua ya makundi.
0 comments:
Post a Comment