London, England.
Nahodha na mlinzi mkongwe wa Chelsea,John Terry,hatashuka dimbani Ijumaa hii kuivaa Liverpool katika mchezo wa ligi kuu ya England hii ni baada ya jeraha la kifundo cha mguu alilolipata Jumapili kwenye mchezo dhidi ya Swansea City kuripotiwa kuwa litamweka nje ya dimba kwa muda wa siku kumi.
Taarifa iliyochapigwa katika mtandao rasmi wa Chelsea imesema leo asubuhi,Terry,alifanyiwa kipimo cha MRI scan ili kubaini ukubwa wa jeraha hilo na kubainika kuwa atahitaji siku kumi kuweza kupona vizuri.
Hii ina maana kwamba sasa Chelsea italazimika kumtumia mlinzi wake mpya David Luiz,27,katika pambano hilo linalotarajiwa kuwa la vuta nikuvute.
0 comments:
Post a Comment