Jinja,Uganda.
ZANZIBAR imetupwa rasmi nje ya michuano ya CECAFA ya wanawake baada ya jioni ya leo kufungwa mabao 9-0 na Uganda katika mchezo wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa Fufa Technical Centre huko Njeru,Jinja (Uganda)
Hii ni mara ya pili kwa Zanzibar kupoteza mchezo kwa mabao mengi katika michuano hiyo kwani katika mchezo wake wa kwanza ilichabangwa mabao 10-1 na Burundi.
Katika mchezo mwingine uliopigwa jioni ya leo Kenya imefuzu nusu fainali baada ya kuwaadhibu Burundi kwa kuwafunga mabao 4-0.
Mabao ya Kenya yamefungwa na Neddy Atieno aliyefunga mara mbili,Esse Akida na nahodha Mary Kinutha waliofunga bao moja kila mmoja.
Ratiba Ijayo.
Kenya v Zanzibar
Uganda v Burundi.
0 comments:
Post a Comment