Barcelona,Hispania.
Bao la kusawazisha la dakika ya 74 la mshambuliaji mkongwe Aritz Aduriz dhidi ya FC Barcelona katika uwanja wa Nou Camp jana usiku limeipa Atletic Bilbao kombe la kwanza baada ya ukame wa miaka 31 baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 katika mchezo wa marudiano wa Super Cup De Espana na matokeo ya jumla kuwa 5-1.
Arduriz alifunga bao hilo akisawazisha bao la mapema la FC Barcelona lililofungwa na Lionel Messi dakika ya 43.FC Barcelona ambayo katika mchezo wa kwanza katika dimba la San Mames ililala kwa kipigo cha bao 4-0 ilipoteza matumaini katika mchezo wa jana baada ya mlinzi wake Gerard Pique kulimwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kuonyesha mchezo usio wa kiungana.
Kufuatia kipigo hicho FC Barcelona imeshindwa kuirudia rekodi iliyoiweka mwaka 2009 pale kocha Pep Guardiola alipokiongoza kikosi hicho kutwaa vikombe sita katika kipindi cha mwaka mmoja pale ilipotwaa Champions League, La Liga,Kombe la Mfalme, European Super Cup,Super Cup de Espana na Klabu bingwa ya dunia.
0 comments:
Post a Comment