Dortmund, Ujerumani.
Liverpool imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga nusu fainali ya michuano ya Europa Ligi baada ya usiku wa kuamkia leo kulazimisha sare ya 1-1 nyumbani kwa Borussia Dortmund huko Westfalenstadion,Signal Iduna Park.
Liverpool ndiyo ilikuwa ya kwanza kubisha hodi langoni mwa mwenyeji kwa bao safi la dakika ya 38 la Divock Origi.Origi alifunga bao hilo akipokea pasi ya James Milner na kumfunga mlinda mlango Roman Weidenfeller.
Kipindi cha pili mlinzi mrefu Mats Hummels aliisawazishia bao Borussia Dortmund kwa kichwa dakika ya 48' akiunganisha mpira wa faulo wa Henrikh
Mkhitaryan
Mechi nyingine za Robo Fainali ya michuano hiyo , Villarreal imeshinda 2-1 dhidi ya Sparta Prague, mabao yote yakifungwa
na Cedric Bakambu dakika ya tatu na 63, huku la wageni likifungwa
na Jakub Brabec dakika ya 49 Uwanja wa El Madrigal.
Sporting Braga imefungwa 2-1 nyumbani na Shakhtar Donetsk Uwanja wa Manispaa mjini Braga.
Mabao ya Shakhtar yamefungwa na Yaroslav Rakitskiy dakika ya 44
na Facundo Ferreyra dakika ya 75,wakati la wenyeji limefungwa na Wilson Bruno Naval Costa Eduardo dakika ya 89.
Athletic Club nayo imefungwa 2-1nyumbani na Sevilla Uwanja wa San
Mames. Mabao ya Sevilla
yamefungwa na Timothee
Kolodziejczak dakika ya 56
na Vicente Iborra dakika ya 83,wakati la wenyeji limefungwa na Aritz Aduriz Zubeldia dakika ya 47.Timu zote zinatarajiwa kurudiana Alhamisi ijayo, Aprili 14
0 comments:
Post a Comment