LIVERPOOL,ENGLAND.
PIGO!!Jordan Henderson hataweza tena kuonekana dimbani msimu huu baada ya jana kuumia goti wakati akiichezea Liverpool katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Europa Ligi dhidi ya Borussia Dortmund ulioisha kwa sare ya bao 1-1.
Henderson,25 aliumia dakika ya 46 na nafasi yake kuchukuliwa na Joe Allen.
Akiongea kuhusu kuumia kwa nahodha wake kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema "Ni bahati mbaya kwa Hendo.Ameumia goti na jeraha ni kubwa.Hatacheza tena msimu huu".
Hii ina maana kuwa Henderson atakosa michezo yote iliyobakia ya ligi kuu nchini England pamoja na ile ya michuano ya Ulaya maarufu kama Europa Ligi huku kukiwa na wasiwasi wa kukosa pia michuano ya Euro 2016 itakayopigwa Ufaransa kuanzia mwezi Juni na kufikia tamati mwezi Julai.
Msimu huu Henderson ameichezea Liverpool michezo 25 na kuifungia mabao mawili huku akikosa michezo kadhaa kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya kisigino.
0 comments:
Post a Comment