728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 24, 2016

    JOSE MOURINHO ADAI BADO YUKO GIZANI

    Singapore

    Jose Mourinho amesema bado yuko gizani kuhusu uwezekano wa siku moja kuwa kocha wa Manchester United lakini anaamini atarudi tena kufundisha mpira katika kipindi kijacho cha majira ya joto.

    Mourinho,53 ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akihusishwa kujiunga na Manchester United tangu alipofutwa kazi katika klabu ya Chelsea mwishoni mwa mwaka jana ameyasema hayo leo wakati akijibu swali aliloulizwa na mwanafunzi mmoja kutoka shule ya Singapore North Light secondary school aliyetaka kujua kama kocha huyo Mreno ataelekea Old Trafford msimu ujao.

    "Sijui chochote,bado niko gizani.Lakini ukweli ni kwamba napenda sana mpira na namiss sana mpira.Nikipata nafasi ya kurudi,nitarudi.Hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

    "Mambo mengi yanasemwa kunihusu.Wapo wanaosema nakwenda China,wengine Italia nakwenda Milan,wengine narudi Inter lakini ukweli ni kwamba kwa sasa sina kazi,sina makubaliano na klabu yoyote na nina furaha kutokuwa na kazi"Alimaliza Mourinho.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JOSE MOURINHO ADAI BADO YUKO GIZANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top