728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, February 11, 2016

    WACHINA NOMA SANA MANOTI YAO YAMNASA EZEQUIEL LAVEZZI

    Paris,Ufaransa.

    Wakati dirisha la usajili nchini China likitarajiwa kufungwa Februari 26 klabu iliyopanda daraja ya Hebei Fortune imeripotiwa kuwa karibu kuinasa saini ya nyota wa PSG Muargentina Ezequiel Lavezzi kwa dau la euro milioni 6.

    Taarifa kutoka Ufaransa zinasema nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 ameshakubaliana kila kitu na Hebei Fortune na kinachosubiriwa sasa ni vipimo vya afya na kumwaga mwino wa kuichezea klabu hiyo.Lavezzi atasaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Hebei Fortune huku akipokea mshahara wa kati ya euero milioni 13-15 kwa mwaka.

    Hivi karibuni Hebei Fortune ilimsajili Gervinho toka AS Roma kwa kitita cha paundi milioni 12.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WACHINA NOMA SANA MANOTI YAO YAMNASA EZEQUIEL LAVEZZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top