Shanghai,China.
Ligi kuu nchini China imeendelea kuwa kivutio kwa nyota wengi wa soka duniani baada ya leo hii Straika Mnigeria Obafemi Martins,31 kujiunga na Shanghai Shenhua akitokea Seattle Sounders kwa dau la dola milioni 3 akitokea Seattle Sounders ya Marekani.
Shanghai Shenhua inakuwa ni klabu ya tisa kwa Martins kujiunga nayo baada ya Reggiana, Inter Milan, Newcastle United, Vfl Wolfsburg,Rubin Kazan na Birmingham City
Akiwa Shangai Shenhua Martins atapata nafasi ya kucheza pamoja na nyota waliotamba Ulaya siku za nyuma kama Fredy Guarin,Giovanni Moreno,Avraam Papadopoulos,Demba Ba,Tim Cahill
Martins alijiunga na Seattle Sounders mwanzoni mwa mwaka 2013 akitokea Levante ya Hispania na kufanikiwa kuifungia mabao 40 na kupika 23 katika michezo 80 ya ligi kuu nchini Marekani (MLS)
0 comments:
Post a Comment