728x90 AdSpace

Saturday, February 27, 2016

INFANTINO NDIYE RAIS MPYA WA FIFA


Zurich,Uswisi.

Katibu Mkuu wa zamani wa UEFA,Gianni Infantino amekuwa Rais wa tisa wa FIFA, baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika jana ijumaa huko Zurich,Uswisi.

Infantino,45 aliibuka mshindi baada ya kujipatia kura 115 huku mpinzani wake wa karibu Sheik Salman akipata kura 88 katika uchaguzi uliolazimika kuingia hatua ya pili baada ya ile ya awali mshindi kushindwa kupatikana kufuatia wagombea wote kushindwa kufikisha nusu ya kura zinazotakiwa.

Infantino ambaye kitaaluma ni Mwanasheria anakuwa ni Mswisi wa pili kushinda Urais wa FIFA, baada ya mtangulizi wake Sepp Blatter.



  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: INFANTINO NDIYE RAIS MPYA WA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown