Cairo,Misri.
Zamalek imetangaza kumfuta kazi kocha wake mkuu Ahmed Hossam ‘Mido’ kufuatia kupokea kichapo cha bao 2-0 toka kwa wapinzani wao wa jadi Al Ahly katika mchezo mkali wa mzunguko wa 17 wa ligi kuu ya Misri uliopigwa jana jumanne huko Cairo.
Kichapo hicho cha jumanne ni cha pili kuikuta Zamalek baada wa wiki iliyopita kulala kwa bao 1-0 toka Ismaily.
Habari za ndani toka Cairo zinadai kuwa baada ya kichapo toka kwa Al Ahly bodi ya Zamalek iliamua kumfuta kazi Mido pamoja na mkurugenzi wake wa michezo Hazem Emam huku Mohamed Salah akipewa jukumu la kuwa kocha wa muda.
Mido alianza kuinoa Zamalek mwezi Januari akichukua nafasi ya Mbrazil Marcos Paquet aliyefutwa kazi kufuatia matokeo mabovu uwanjani.
0 comments:
Post a Comment