728x90 AdSpace

Saturday, February 13, 2016

MRITHI WA JOHN TERRY CHELSEA SASA HADHARANI

London,England.

Klabu ya Chelsea imeripotiwa kuanza mapema kujiandaa na maisha bila ya mlinzi na nahodha wake John Terry baada ya taarifa toka vyombo mbalimbali vya habari kuripoti kuwa miamba hiyo ya jiji la London inajipanga kumsajili mlinzi kisiki wa Atletico Madrid Mruguayi Diego Godin.

Habari za ndani kabisa zinadai Chelsea imemchagua Godin kwa kuwa ana sifa zinazofanana sana na zile za John Terry ambazo ni ukakamavu,uhamasishaji na uongozi uwanjani.Godin ndiye nahodha wa Atletico Madrid.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MRITHI WA JOHN TERRY CHELSEA SASA HADHARANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown