Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetoa ratiba ya
kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini
ya miaka 17 (U-17) zitakazofanyika nchini Madagascar mwakani kwa timu
ya Taifa ya Tanzania (Serengeti Boys) kuanza na Shelisheli.
Katika ratiba hiyo iliyotolewa makao makuu ya CAF, Cairo Misri na
nakala yake kutumwa kwa TFF, Tanzania imepangwa kucheza mchezo wa kwanza
dhidi ya Shelisheli kati ya Juni 24,25,26 nchini na marudaino kuchezwa
Julai 01,02,03 nchini Shelisheli.
Mshindi kati ya mchezo huo namba 15 na16 atacheza dhdi ya timu ya
Taifa ya Afrika Kusini katika hatua inayofuata ya 16 bora, na kisha
baadae kupata timu 8 zitakazofuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika
nchini Madagascar mwakani.
Fainali za Kombe la Dunia (FIFA U17) kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwezi Septemba waka 2017 nchini India.
0 comments:
Post a Comment