JOEL MATIP amekubali kujiunga na Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kuripotiwa kusaini mkataba wa awali utakaomfanya atue Anfield kama mchezaji huru akitokea Shalke O4 ya Ujerumani.
Matip,24 ambaye ni raia wa Cameroun mwenye uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kati na kiungo mkabaji kwa kipindi kirefu amekuwa akindwa na Kocha Jurgen Klopp kuja kuimarisha safu ya ulinzi ya Liverpool na sasa mambo yameenda vizuri baada ya nyota huyo aliyefunga mabao matatu msimu huu kusaini mkataba wa awali wa kukipiga Anfield msimu ujao.
Wakati Matip akija Liverpool mlinzi mkongwe Kolo Toure,35 anatarajiwa kutupiwa virago mwishoni mwa msimu huu ili kupisha damu changa.
0 comments:
Post a Comment