Manchester,England.
Klabu ya Manchester United imemteua kiungo wake wa zamani Nicky Butt kuwa mkuu wake mpya wa shule yake ya kunoa vipaji vya soka vya klabu hiyo.[Akademi].
Butt,41amepewa nafasi hiyo nyeti baada ya Brian McClair kujiuzuru Juni mwaka jana na kuiacha nafasi hiyo wazi.Butt ambaye kwa kipindi cha miaka minne sasa amekuwa akiwanoa wachezaji wachanga,jukumu lake kubwa litakuwa ni kuhakikisha Manchester United inazalisha nyota wengi kutoka katika timu zake za jana na kurudisha falsafa ya klabu iliyoanza kupotea.
Butt aliichezea Manchester United michezo 387 akifanikiwa kutwaa mataji sita ya ligi kuu,mataji matatu ya FA Cup na moja la ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 1999.
0 comments:
Post a Comment